Serikali imesema itakuja bajeti mahususi kwa ajili ya kurekebisha barabara zote nchini zilizoathiriwa na mvua. Pia, imesema inaelewa bajeti ya Wizara ya Ujenzi ya Sh1.7 trilioni ni ndogi na kwamba atakapokuja kusoma bajeti kuu hilo litakuwa limeangaliwa.
Hayo yamesemwa leo Alhamisi Mei 30, 2024 na Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia bajeti ya Wizara ya Ujenzi.
“Serikali kuja na bajeti mahsusi ya kurejesha barabara zilizogaribika wakati wa mvua. Urakarabti wa barabara hizo unahitaji kati ya Sh700 bilioni na Sh1 tirilioni kwa barabara za Tanroads (Wakala wa barabara Tanzania) na Sh300 bilioni kwa barabara za Tarura (Wakala ya Barabara Vijijini na Mijini).
“Serikali imetumia takriban Sh40 trilioni kuwekeza kwenye barabara, Serikali haiwezi kukubali kupoteza fedha hizo ambazo imewekeza,” amesema.
Pia, Mwigulu amezungumzia kutotekelezwa mradi wa ujenzi wa barabara saba za kiwango cha lami zenye jumla ya kilometa 2,035 kwa kutumia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F) ndani ya mwaka mmoja.