Wakazi wa Kisiwa cha Kome wilayani Sengerema wameiomba Serikali kuwawekea kivuko, Kisiwa hicho chenye watu zaidi ya 20,000 wanaojihusisha na shughuli za uvuvi kinahudumiwa na kivuko cha MV Kome II chenye uwezo wa kubeba abiria 120 na tani 40 za mizigo.
Wakizungumza na Mwananchi Digital wakazi hao wamesema kutokana na changamoto ya usafiri kati ya kijiji cha Nyakalilo na kisiwa cha Kome baadhi ya wakazi wake wanalazimika kutumia mitumbwi kuvuka ndani ya ziwa hilo jambo linalohatarisha maisha yao.