Hatua ya Serikali kuzuia uvuvi wa samaki aina ya kambamiti (prawns) kuanzia Septemba 2018 hadi Machi 2019 na ukataji wa miti ya mikoko kwa ajili ya biashara, imezua sintofahamu kwa wakazi wa vijiji vya Kiomboni, Mchinga, Mfisini, na Nyamisati vyote vikiwa ndani ya Kata ya Salale, Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani.